Zaburi 44

Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo.

Psalm 44:4 (UKJV) You are my King, O God: command deliverances for Jacob.

2Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu.

3Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.

4Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo.

5Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.

6Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi;

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.