3Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.
4Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo.
5Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.
6Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi;
7bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, unawaaibisha watesi wetu.