5Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.
6Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi;
7bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, unawaaibisha watesi wetu.
8Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, nasi tutalisifu jina lako milele.
9Lakini sasa umetukataa na kutudhili, wala huendi tena na jeshi letu.