15Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake.
16Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka,
17kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye.
18Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,
19atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.