4Wewe si Mungu unayefurahia uovu, kwako mtu mwovu hataishi.
5Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya.
6Unawaangamiza wasemao uongo. Bwana huwachukia wamwagao damu na wadanganyifu.
7Lakini mimi, kwa rehema zako kuu, nitakuja katika nyumba yako, kwa unyenyekevu, nitasujudu kuelekea Hekalu lako takatifu.
8Niongoze katika haki yako, Ee Bwana, kwa sababu ya adui zangu, nyoosha njia yako mbele yangu.