10Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
11Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
12Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze.
13Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.
14Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.