9Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote.
10Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
11Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
12Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze.
13Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.