7Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi.
9Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote.
10Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
11Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.