5Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.
6Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni, ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.
7Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi.
9Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote.