1Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu.
2Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu.
3Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
4Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, na kuwa na haki utoapo hukumu.