20Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata.
21Waliweka nyongo katika chakula changu na walinipa siki nilipokuwa na kiu.
22Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, nayo iwe upatilizo na tanzi.
23Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima.
24Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate.