22Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, nayo iwe upatilizo na tanzi.
23Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima.
24Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate.
25Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao.
26Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.