24Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate.
25Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao.
26Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.
27Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako.
28Wafutwe kutoka kitabu cha uzima na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki.