8Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.
9Usinitupe wakati wa uzee, wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.
10Kwa maana adui zangu wananisengenya, wale wanaonivizia kuniua wafanya hila.
11Wanasema, “Mungu amemwacha, mkimbilieni mkamkamate, kwani hakuna wa kumwokoa.”
12Ee Mungu, usiwe mbali nami, njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.