11Wanasema, “Mungu amemwacha, mkimbilieni mkamkamate, kwani hakuna wa kumwokoa.”
12Ee Mungu, usiwe mbali nami, njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.
13Washtaki wangu na waangamie kwa aibu, wale wanaotaka kunidhuru na wafunikwe kwa dharau na fedheha.
14Lakini mimi, nitatumaini siku zote, nitakusifu zaidi na zaidi.
15Kinywa changu kitasimulia haki yako, wokovu wako mchana kutwa, ingawa sifahamu kipimo chake.