Zaburi 71

Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara.

Psalm 71:7 (UKJV) I am as a wonder unto many; but you are my strong refuge.

5Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.

6Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima.

7Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara.

8Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.

9Usinitupe wakati wa uzee, wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.