Zaburi 73

Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi.

Psalm 73:14 (UKJV) For all the day long have I been plagued, and chastened every morning.

12Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri.

13Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.

14Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi.

15Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.

16Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.