19Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho!
20Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto.
21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu,
22nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.
23Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.