21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu,
22nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.
23Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.
24Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu.
25Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.