23Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.
24Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu.
25Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.
26Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.
27Wale walio mbali nawe wataangamia, unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.