2Kumbuka watu uliowanunua zamani, kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: Mlima Sayuni, ambamo uliishi.
3Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.
4Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi, wanaweka bendera zao kama alama.
5Walifanya kama watu wanaotumia mashoka kukata kichaka cha miti.
6Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa kwa mashoka na vishoka vyao.