9Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”
10Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.”
11Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.
12Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.
13Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?