Zaburi 77

Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.

Psalm 77:12 (UKJV) I will meditate also of all your work, and talk of your doings.

10Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.”

11Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.

12Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.

13Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

14Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.