Zaburi 77

Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

Psalm 77:14 (UKJV) You are the God that do wonders: you have declared your strength among the people.

12Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.

13Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

14Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

15Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu.

16Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.