58Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.
59Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa.
60Akaiacha hema ya Shilo, hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.
61Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui.
62Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake.