Zaburi 78

Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.

Psalm 78:65 (UKJV) Then the LORD awaked as one out of sleep, and like a mighty man that shouts by reason of wine.

63Moto uliwaangamiza vijana wao, na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,

64makuhani wao waliuawa kwa upanga, wala wajane wao hawakuweza kulia.

65Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.

66Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele.

67Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, hakulichagua kabila la Efraimu,

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.