65Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.
66Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele.
67Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, hakulichagua kabila la Efraimu,
68lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda.
69Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele.