Zaburi 78

Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.

Psalm 78:70 (UKJV) He chose David also his servant, and took him from the sheepfolds:

68lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda.

69Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele.

70Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.

71Kutoka kuchunga kondoo alimleta kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, wa Israeli urithi wake.

72Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.