7Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake.
8Ili wasifanane na baba zao, waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake, ambao roho zao hazikumwamini.
9Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita.
10Hawakulishika agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake.
11Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonyesha.