9Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita.
10Hawakulishika agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake.
11Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonyesha.
12Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, huko Soani, katika nchi ya Misri.
13Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta.