10Hawakulishika agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake.
11Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonyesha.
12Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, huko Soani, katika nchi ya Misri.
13Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta.
14Aliwaongoza kwa wingu mchana na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha.