14Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote! Tazama chini kutoka mbinguni na uone! Linda mzabibu huu,
15mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, mwana uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
16Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto, unapowakemea, watu wako huangamia.
17Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume, mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
18Ndipo hatutakuacha tena, utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.