17Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu.
18Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
19Ulizungumza wakati fulani katika maono, kwa watu wako waaminifu, ukasema: “Nimeweka nguvu kwa shujaa, nimemwinua kijana miongoni mwa watu.
20Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimemtia mafuta yangu matakatifu.
21Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu.