24Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.
25Nitauweka mkono wake juu ya bahari, mkono wake wa kuume juu ya mito.
26Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’
27Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.
28Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara.