38Lakini wewe umemkataa, umemdharau, umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.
39Umelikana agano lako na mtumishi wako, na umeinajisi taji yake mavumbini.
40Umebomoa kuta zake zote, na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.
41Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; amekuwa dharau kwa jirani zake.
42Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, umewafanya watesi wake wote washangilie.