41Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; amekuwa dharau kwa jirani zake.
42Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, umewafanya watesi wake wote washangilie.
43Umegeuza makali ya upanga wake, na hukumpa msaada katika vita.
44Umeikomesha fahari yake, na kukiangusha kiti chake cha enzi.
45Umezifupisha siku za ujana wake, umemfunika kwa vazi la aibu.