Zaburi 90

Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu, kulingana na miaka tuliyotaabika.

Psalm 90:15 (UKJV) Make us glad according to the days wherein you have afflicted us, and the years wherein we have seen evil.

13Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini? Wahurumie watumishi wako.

14Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma, ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote.

15Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu, kulingana na miaka tuliyotaabika.

16Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, utukufu wako kwa watoto wao.

17Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu; uzithibitishe kazi za mikono yetu: naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.