11Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako? Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako.
12Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili tujipatie moyo wa hekima.
13Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini? Wahurumie watumishi wako.
14Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma, ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote.
15Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu, kulingana na miaka tuliyotaabika.