2Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
3Huwarudisha watu mavumbini, ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.”
4Kwa maana kwako miaka elfu ni kama siku moja iliyokwisha pita, au kama kesha la usiku.
5Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo, nao ni kama majani machanga ya asubuhi:
6ingawa asubuhi yanachipua, ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka.