1Bwana, wewe umekuwa makao yetu katika vizazi vyote.
2Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
3Huwarudisha watu mavumbini, ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.”
4Kwa maana kwako miaka elfu ni kama siku moja iliyokwisha pita, au kama kesha la usiku.