1Wimbo ulio bora wa Solomoni.
2Unibusu kwa busu la kinywa chako, kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.
3Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!
4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!
5Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni.