7Umbo lako ni kama la mtende, nayo matiti yako kama vishada vya matunda.
8Nilisema, “Nitakwea mtende, nami nitayashika matunda yake.” Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu, harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa,
9na kinywa chako kama divai bora kuliko zote. Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu, ikitiririka polepole juu ya midomo na meno.
10Mimi ni mali ya mpenzi wangu, nayo shauku yake ni juu yangu.
11Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani, twende tukalale huko vijijini.