39Azaria akamzaa Helesi, Helesi akamzaa Eleasa,
40Eleasa akamzaa Sismai, Sismai akamzaa Shalumu,
41Shalumu akamzaa Yekamia, naye Yekamia akamzaa Elishama.
42Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa: Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
43Hebroni alikuwa na wana wanne: Kora, Tapua, Rekemu na Shema.