1 Wakorintho 12

Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

1 Corinthians 12:19 (UKJV) And if they were all one member, where were the body?

17Kama mwili wote ungelikuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, kunusa kungekuwa wapi?

18Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda.

19Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20Kama ulivyo, una viungo vingi, lakini mwili ni mmoja.

21Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.