1 Wakorintho 9

Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu.

1 Corinthians 9:3 (UKJV) Mine answer to them that do examine me is this,

1Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana?

2Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni mhuri wa utume wangu katika Bwana.

3Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu.

4Je, hatuna haki ya kula na kunywa?

5Je, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini, kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.