2 Nyakati 6

“Sasa inuka, Ee Bwana Mungu, na uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Ee Bwana Mungu, na wavikwe wokovu, watakatifu wako na wafurahi katika wema wako.

2 Chronicles 6:41 (UKJV) Now therefore arise, O LORD God, into your resting place, you, and the ark of your strength: let your priests, O LORD God, be clothed with salvation, and let your saints rejoice in goodness.

39basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na kuitetea haki yao. Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako.

40“Sasa, Mungu wangu, macho yako na yafumbuke na masikio yako yasikie maombi yaombwayo mahali hapa.

41“Sasa inuka, Ee Bwana Mungu, na uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Ee Bwana Mungu, na wavikwe wokovu, watakatifu wako na wafurahi katika wema wako.

42Ee Bwana Mungu, usimkatae mpakwa mafuta wako. Kumbuka upendo mkuu uliomwahidia Daudi mtumishi wako.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.