20Je, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru: giza nene, bila mwonzi wa mwanga?
21“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini; siwezi kuvumilia makusanyiko yenu.
22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka, sitazikubali. Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani, sitazitambua.
23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.
24Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!