Amosi 5

Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!

Amos 5:24 (UKJV) But let judgment run down as waters, and righteousness as a mighty stream.

22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka, sitazikubali. Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani, sitazitambua.

23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.

24Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!

25“Je, mliniletea dhabihu na sadaka kwa miaka arobaini kule jangwani, ee nyumba ya Israeli?

26Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu, Sikuthi mungu wenu mtawala, na Kiuni mungu wenu wa nyota, ambao mliwatengeneza wenyewe.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.