Amosi 5

Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.

Amos 5:23 (UKJV) Take you away from me the noise of your songs; for I will not hear the melody of your viols.

21“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini; siwezi kuvumilia makusanyiko yenu.

22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka, sitazikubali. Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani, sitazitambua.

23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.

24Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!

25“Je, mliniletea dhabihu na sadaka kwa miaka arobaini kule jangwani, ee nyumba ya Israeli?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.