25Barabarani upanga utawakosesha watoto; nyumbani mwao hofu itatawala. Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia, pia watoto wachanga na wazee wenye mvi.
26Nilisema ningewatawanya na kufuta kumbukumbu lao katika mwanadamu.
27Lakini nilihofia dhihaka za adui, adui asije akashindwa kuelewa, na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; Bwana hakufanya yote haya.’ ”
28Wao ni taifa lisilo na akili, hakuna busara ndani yao.
29Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili, na kutambua mwisho wao utakuwa aje!